Jumanne , 26th Oct , 2021

Watu wawili wamepoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya basi la abiria la kampuni ya Kimotco ya jijini Arusha, ajali ambayo imetokea leo Oktoba 26, 2021, majira ya saa 1:00 asubuhi katika barabara ya Arusha-Babati, eneo la Makuyuni wilayani Monduli mkoani Arusha.

Basi la kampuni ya Kimotco lililopata ajali

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo, amesema kuwa majeruhi wanne walikuwa na hali mbaya, na walipelekwa katika hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya matibabu.