Alhamisi , 4th Sep , 2025

Mahakama ya wilaya ya Itilima iliyopo mkoani Simiyu imemhukumu Yosia Paulo Magembe (20) mkazi wa kijiji cha Sunzula kilichopo wilayani humo kwenda jela miaka30 kwa kukutwa na hatia ya makosa matatu.

Mahakama ya wilaya ya Itilima iliyopo mkoani Simiyu imemhukumu Yosia Paulo Magembe (20) mkazi wa kijiji cha Sunzula kilichopo wilayani humo kwenda jela miaka30 kwa kukutwa na hatia ya makosa matatu.

Kosa la kwanza ni kutorosha binti mwenye umri chini ya wa miaka 16 kinyume na kifungu cha 134 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2023 huku kosa la pili likiwa ni ni kubaka kinyume na kifungu cha 130(1)(2)(e) na 131(1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyo fanyiwa marejeo mwaka 2023 na kosa la tatu kumpa mimba mwanafunzi kinyume na kifungu cha 62(3) cha sheria ya elimu sura ya 353 kama ilivyo fanyiwa marejeo mwaka 2023 .

Hukumu ya shauri la jinai Na.19541/2025 imesomwa mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa wilaya ya Itilima Roberth Kaanwa.