Kibatala amesema kuwa kabla ya leo walishaandika barua ya kujitoa kwenye kesi yao na kwamba Wema alitakiwa kuwatambulisha Mawakili wake wapya siku ambayo kesi yake itasikilizwa (Leo).
Kibatala amesema pia wameiomba radhi mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi Kisutu kama yapo makwaruzano yaliyowahi kutokea wakati akiwa anamtetea mteja wao huyo na mahakama iwasamehe kwani ni katika kutimiza wajibu wa kazi.
Hata hivyo Mwanasheria Alberto Msando ametangazwa kama Wakili mpya wa Wema Sepetu baada ya Kibatala kujiengua na kwamba ataanza kumuwakilisha Februari 8
Mpaka sasa Kibatala anapoacha kuwa wakili wa Wema Sepetu tayari mashahidi wawili walishasikilizwa.
Wema Sepetu anashtakiwa kwa kosa kukutwa na dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na kutumia.