Aliyesaidiwa na Mkuu wa Majeshi atoa neno

Jumapili , 9th Aug , 2020

Mwanajeshi wa Kikosi cha Jeshi namba 833 Oljoro Arusha, Tete Mwaipaya, amemshukuru Mkuu wa Majeshi nchini Venance Mabeyo kwa kumpa nafasi ya kuingia jeshini kwa kuwa kabla ya nafasi hiyo alikuwa ni mwanasarakasi wa kucheza na  Baiskeli katika matamasha mbalimbali.

Kushoto ni Tete Mwaipaya na kulia ni Mkuu wa Majeshi nchini Venance Mabeyo.

Kauli hiyo ameitoa hivi karibuni wakati akifanya mazungumzo maalumu na EATV, na kusema kuwa nafasi hiyo aliitafuta kwa muda mrefu lakini hakuweza kuipata.

"Shughuli zangu zilikuwa ni hizi za Sarakasi nazunguka mikoa mbalimbali, kuna siku kulikuwa na sherehe Msasani Beach ya wanajeshi sasa alikuwepo Mkuu wa Majeshi pale nilionesha kipaji changu na ndipo alipoweza kuniona akasema huyu kijana aajiriwe jeshini" amesema Tete.

Tazama video hapa chini