
Kitanda cha Mbao.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo na mamlaka hiyo imemuomba radhi abiria huyo kwa tukio hilo na usumbufu uliojitokeza, huku ikieleza kuwa haina nia ya kuzuia utengenezaji, usafirishaji na matumizi ya samani.
“Afisa wetu alishindwa kutafsiri masharti ya kifungu na mahitaji ya utoaji wa hati ya usafirishaji kwani kama msafirishaji binafsi kwa matumizi ya nyumbani asingeweza kukidhi vigezo vya kuwa na hati hiyo,”imesema taarifa hiyo.
Kutokana na hatua hiyo, TFS imebainisha kuwa hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa Kanuni za utumishi wa umma dhidi ya mtumishi aliyehusika na utoaji wa lugha isiyo na staha wakati akitekeleza sheria ya misitu ambapo alitegemewa kutoa elimu stahiki kwa umma.