Jumatano , 29th Jun , 2022

Ibrahimu Nicodems (22), ameuawa baada ya kuchomwa kisu na binamu yake aitwaye Thomasi Amsii mkazi wa Mtaa wa Sawe wilaya ya Babati mkoani Manyara, kwa sababu ya wivu wa mapenzi ambapo mtuhumiwa amesema alimkuta marehemu yupo na mke wake chumbani wakishiriki tendo la ndoa.

Kisu

EATV imezungumza na Mwenyekiti wa wa mtaa huo Michael John alikiri kutokea kwa tukio hilo kwenye mtaa wake na kusema kuwa baada ya kutokea kwa mauaji hayo alichukua jukumu la kuzungumza na mtuhumiwa sababu ya kuchukua jukumu la kumuuwa binamu yake na kusema alimkuta marehemu yupo na mke wake chumbani wanafanya mapenzi.

Kwa upande wake Mama wa marehemu aitwaye Agnes Yona, ambaye amelaani tukio hilo kwa kuwa marehema na mtuhumiwa ni mtu na ndugu yake.