Jumatatu , 18th Aug , 2025

Waandamanaji wengi wamejitokeza katika maeneo mbalimbali kote nchini Israel wakiishinikiza serikali kusitisha vita na kundi la Hamas na kuwarejesha nyumbani mateka wanaoshikiliwa katika Ukanda wa Gaza.

Maandamano hayo yaliyoanza Jumapili asubuhi yanaupinga pia mpango wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa kuvitanua zaidi vita katika Ukanda wa Gaza.

Wakati huohuo wawakilishi wa kundi la Hamas wamelipokea pendekezo jipya la kusitisha vita kwa siku sitini Ukanda wa Gaza na kuachiliwa kwa mateka katika awamu mbili.

 Afisa kutoka kundi hilo aliyeomba kutokutajwa jina amesema pendekezo hilo linalosubiri kupitiwa na Hamas linatoa njia ya kuanzishwa kwa majadiliano yatakayovimaliza kabisa vita vya Gaza.