Jumatano , 19th Apr , 2023

Mahakama ya wilaya ya Kilwa imemhukumu Muharami Hassan Nayonga, kifungo cha miaka 30 jela baada ya kumkuta na hatia ya kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile na watu mbalimbali.

Muharami Hassan Nayonga

Muharami ambaye ni mlinzi wa SUMA JKT na mkazi wa Kata ya Masoko, alikamatwa Aprili 13, 2023, baada ya kumshawishi kwa kutumia simu, kijana anayefahamika kwa jina la Zalafi Selemani ili aweze kumuingilia kinyume na maumbile.

Baada ya kukamatwa, mtuhumiwa alichunguzwa na wataalamu wa Afya ambao walibaini kuwa kijana huyo hushiriki ngono kinyume na maumbile.

Mtuhumiwa alifikishwa mahakamani na kukiri makosa yake na ndipo jamhuri ilipomhukumu kifungo cha miaka 30 jela.
Hukumu hiyo ya kesi namba 27 ya mwaka 2023 imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Carolina Mtui, ikiwa ni baada ya kumkuta na hatia juu ya kosa hilo ambalo lipo kinyume na kifungu namba 154, kifungu kidogo cha kwanza, sheria ya kanuni ya Adhabu, sura namba 16.