Alhamisi , 20th Jan , 2022

Mara baada ya picha za askari wa usalama barabarani kusambaa mitandaoni zikimuonesha akiwa ameshika fedha zinazodaiwa kuwa ni za rushwa, Jeshi la Polisi nchini limesema kuwa ushahidi utakapopatikana hatua zitachukuliwa.

Kushoto ni Askari anayefuatiliwa na kulia ni Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini SACP David Misime

Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 20, 2022, na Msemaji wa Jeshi hilo SACP David Misime, ambapo amesema mara baada ya picha hizo kusambaa mitandaoni hatua zilianza kuchukuliwa kwa kushirikiana na wadau wengine.

"Hakuna aliyepo juu ya sheria, hivyo hatua kali na stahiki kwa mujibu wa sheria, kanuni, taratibu na ushahidi utakaopatikana zitachululiwa," amesema SACP Misime.