Jumanne , 9th Mei , 2023

Aneth Edward mkazi wa mtaa wa Mji Mpya Kawe Dar es Salaam, amewaomba Watanzania wamsaidie kupata fedha za matibabu ya mtoto wake Brian Karua, anayesumbuliwa na maradhi ya kichwa yaliyopelekea kuanza kupooza kwa mwili wake na hawezi kula wala kujihudumia kwa chochote.

Brian Karua,

EATV imefika nyumbani kwa Bi. Aneth anayeishi na mtoto wake ambaye kwa takribani miaka 13 amekuwa akisumbuliwa na maradhi hayo ya kichwa. Mawasiliano ni 0693 217 101 

Mama mzazi wa Brian Karua anasimulia historia ya ugonjwa wa mtoto wake, kuwa alianza kuumwa na kichwa akiwa kidato cha pili, na baadaye alianza kuonesha dalili za kuchanganyikiwa na kuanza kupooza viungo.

Bi Aneth anasimulia kuwa amehangaika kutafuta utatuzi wa afya ya mtoto wake, bila kupata suluhisho la afya ya kijana huyo, licha ya baba wa mtoto huyo kuwatelekeza.

Mama huyu pia amesema aliamua  kuacha kazi aliyokuwa akiifanya ili aweze kumhudumia mtoto wake ambaye hawezi kujihudumia mwenyewe, huku sasa akiomba msaada wa watanzania kwani uwezo wake umefika mwisho.