
Waziri wa TAMISEMI, Seleman Jaffo
Akitoa taarifa hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Seleman Jaffo, ameeleza kuwa Mkurugenzi huyo alikuwa hazingatii miongozo na taratibu za manunuzi.
"Imeonekana wazi kwamba Mkurugenzi huyu alinunua sumu ya kupulizia mchwa kwa ajlili ya majengo kwa kiasi cha sh milioni 66, ni zaidi ya matarajio ya matumizi ya fedha katika eneo hilo'', amesema Waziri Jaffo.
Hivi sasa atakayekaimu nafasi hiyo ya ukurugenzi ni Mhandisi Godfrey Mlowe, ambaye ni Meneja wa TARURA katika Halmashauri hiyo na kwamba atasimamia ukamilishaji wa majengo ya Hospitali pamoja na ujenzi wa vituo vya afya vya Mikese na Kinonko.