Jumatatu , 24th Apr , 2023

Mahakama ya wilaya ya Kiteto mkoani Manyara imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Yohana Lazaro (58) mkazi wa Kijiji cha Azimio Kata ya Matui kwa kosa la kubaka mtoto mdogo wa shule ya msingi

Kesi hiyo ya ubakaji namba 64.2022 iliyokuwa iliyokuwa inamkabili Yohana Lazaro (58) imemalizika leo kwa mtuhumiwa huyo kupewa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela

Awali ilielezwa mahakamani hapo hapo kuwa mtuhumiwa huyo kwa nyakati tofauti kuanzia Machi na Desemba 2021 katika kijiji cha Azimio alikuwa na tabia ya kumbaka mtoto huyo mdogo

Mtuhumiwa  alifikishwa mahakama ya wilaya ya Kiteto Juni 27.2022 kwa kosa hilo la ubakaji na kusomewa shtaka ambapo awali alikana  kosa hilo kisha hakimu wa mahakama hiyo Mosi Sasy kuanza kuisikiliza pande hizo mbili 

Hakimu Sasy baada ya kukamilika kwa ushahidi wa pande hizo mbili alisema mahakama pasina shaka ilibaini kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo

Mtuhumiwa hakuwa na cha kujitetea hivyo hakimu Mossi Sasy alimtia hatiani kifungo cha kwenda jela miaka 30
Imeelezwa kuwa mtuhumiwa alitenda kosa kinyume na kifungu cha 130 (1) na (2) (e) na kifungu cha 131 (1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16