
Kamishna Ahmed Msangi
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamishna wa Polisi DCP Ahmed Msangi amesema kuwa majira ya saa 10:15 asubuhi katika kijiji cha Muriti wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza, mwanamume aliyefahamika kwa jina la Melkiad Misana alifariki dunia wakati akikimbizwa hospitali baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali mgongoni baada ya kuzuka kwa ugomvi kati yao kisha kuchomana na vitu vyenye ncha kali, kitendo ambacho ni kosa la jinai.
Akiendelea kufafanua kuhusiana na kifo hicho Kamishna Msangi amesema "Inadaiwa kuwa usiku marehemu hakulala nyumbani kwake lakini alirudi nyumbani asubuhi akiwa amelewa kitendo ambacho hakikumfurahisha mkewe bi Bukhehere Willium. kutokana na hali hiyo wawili hao walijikuta wakiingia kwenye ugomvi kisha kuanza kupigana kwa kutumia vitu vyenye ncha kali kwa kila mmoja kumchoma mwenzake kwenye maeneo tajwa hapo juu, hali iliyopelekea kila mmoja baada ya muda mchache kupita kupoteza fahamu" - Kamishna Msangi.
Msikilize hapa chini Kamisha Msangi akifafanua.