
Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali Mstaafu Prof. Mussa Assad.
Prof Assad amesema siku ambayo inadaiwa alichukuliwa na watu wasiojulikana, alikuwa kwenye hafla ya kidini wilayani Kisarawe.
"Kilichotokea jana nadhani ni kutoelewana tu, mimi nilialikwa na taasisi moja inayoitwa TANPO, kule nilipokwenda ilikuwa mbali sana, kuna changamoto ya kuwepo kwa mtandao, lakini mimi nilikuwa sawa kabisa" amesema Profesa Assad.
Aidha Profesa Assad, amewataka watu kueleza jambo kama wanaliona haliko sawa, na si kulikalia kimya ili kuondoa sintofahamu.