Jumanne , 15th Aug , 2017

Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania aliyemaliza muda wake hapa  Mhe. Jaap Frederiks  ameahidi kurudi nchini mara kwa mara kufanya matembezi kwani amevutiwa na wema wa Watanzania pamoja na vivutioo vya utalii.

Balozi wa Uholanzi Jaap Frederiks akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu

Balozi huyo ameyasema hayo leo alipokutana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipofika Ikulu kwa lengo la kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini. 

Makamu wa Rais alimhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itazidi kuimarisha uhusiano wake na nchi ya Uholanzi hasa katika sekta  ya kilimo, elimu na uboreshwaji  wa  mazingira ya uwekezaji ili  kufikia lengo la Tanzania ya Viwanda.

Mh. Balozi ameahidi kwenda kuwa mjumbe mzuri huko anapoelekea ikiwa ni pamoja na kutangaza vivutio vilivyopo nchini.