Jumatatu , 6th Mar , 2023

Mamlaka nchini Bangladesh inachunguza chanzo cha moto mkubwa katika kambi ya wakimbizi ya Rohingya ambayo imesababisha watu 12,000 kukosa makazi.

Hakuna majeruhi walioripotiwa, lakini moto huo siku ya Jumapili uliteketeza makazi 2,000 baada ya kusambaa haraka kupitia mitungi ya gesi jikoni, maafisa walisema.

Polisi wanachunguza iwapo moto huo ulikuwa kitendo cha uhujumu uchumi. Mtu mmoja amekamatwa, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti. Kambi hiyo iliyoko kusini mashariki inaaminika kuwa kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani.

Wengi wa wakaazi wake zaidi ya milioni moja, wakimbizi wa Rohingya, walikuwa wamekimbia mateso katika nchi jirani ya Myanmar.

Siku ya Jumatatu, mamia walikuwa wamerejea katika eneo la Cox's Bazar kuona kile wanachoweza kuokoa kutoka kwa magofu hayo. Moto huo umeteketeza makazi yaliyojengwa na  mianzi na lami, afisa mmoja alisema.

Moto huo ulidhibitiwa ndani ya saa tatu lakini takriban misikiti 35 na vituo 21 vya kujifunza kwa wakimbizi hao pia viliharibiwa,