Jumatatu , 28th Mar , 2016

Mkutano wa Kwanza wa wa Baraza la wawakilishi visiwani Zanzibar, unatarajiwa kuanza March 30 mwaka huu bila ya kambi pinzani kuwapo baada ya chama cha CUF, kususia uchaguzi mkuu wa marudio visiwani humo.

Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Dkt. Yahaya Khamis Hamad

Akizungumza na waandishi wa habari jana visiwani Zanzibar Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Dkt. Yahaya Khamis Hamad amesema matayarisho ya kikao hicho yamekamilika ambapo siku hiyo kazi kubwa itakayofanyika itakua ni kumchagua Spika.

Amesema mpaka sasa barazac hilo limepokea fomu moja ya mgombea kutoka Chama cha Mapinduzi(CCM), Mhe. Zuberi Ali Maulid ambae amependekezwa na chama chake kuwana wadhifa huo.

Hamas amesema kuwa Baraza la Wawakilishi liliiandikia Tume ya Uchaguzi Zanzibar, (ZEC), barua ya nafasi ya uspika na kuvitaarifu vyama vya siasa lakini vimeshindwa kujitokeza mpaka muda umemalizika wa kuchukua fomu.