Jumatatu , 27th Feb , 2023

Zaidi ya shilingi bilioni 231 zinatarajiwa kutumika kujenga mradi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi BRT awamu ya tatu katika barabara ya Nyerere kuelekea Gongo la mboto yenye urefu wa kilometa 23.3 

Ujenzi huo utaifanya njia hiyo kuwa na jumla ya njia sita hali itakayo punguza msongamano wa magari katika barabara hiyo.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam alipotenbelea eneo la mradi pamoja na kambi ya mkandarasi wa mradi huo waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema mradi huo utakaokamilika mwezi April mwakani utajengwa kwa kiwango cha zege ikiwa ni mpango wa serikali katika kukabiliana na foleni katika barabaravza jiji la Dar es salaam.

Kwa upande wake meneja wa Tanroads mkoa wa Dar es salaam Harun Senkuku amesema wao kama wasimamizi wa mradi huo watahakikisha wanasimamia mradi huo uweze kutekelezwa kwa muda uliopangwa ambao ni miezi 20 huku akielezea maendeleo ya ujenzi wa mradi wa BRT awamu ya pili katika barabra ya kimara ambao unategemewa kukamilika mwezi April mwaka huu

Kwa upande wake meneja wa miradi ya BRT kutoka Tanroads Elibariki Mmari amesema nje ya mradi huo wa barabara ya Nyerere zamani Pugu kuanza ujenzi pia wanakamilisha ujenzi katika barabara ya Mbagala, Kimara, .Posta na barabara ya Ali Hassanmwinyi huku pia wakitegemea kujenga mradi huo katika barabara ya Tegeta, .Mandela na Kigogo kupitia dampo mpaka tabata ili kukabiliana na changanoto ya foleni

Katika ziara hiyo profes a mbarawa amekagua vifaa vya ujenzi wa mradi huo katika kambi ya mkandarasi ambapo ameshuhudia ujenzi wa makaravati yatakayowekwa katika ujenzi wa barabara ya mwendokasi ambapo makaravati hayo yote yana jumla ya urefu wa kilometa 50. Ukijengwa na kampuni ya synohydro