Jumanne , 4th Apr , 2023

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange amesema Katika Mwaka wa Fedha wa 2023/24 Serikali imetenga bajeti ya shilingi bilioni 8.75 kwa ajili ya ujenzi, upanuzi na ukamilishaji wa vituo vya afya 20 katika halmashauri

Amesema hayo leo tarehe 04 Aprili 2023  Bugeni Dodoma wakati akijibu Swali la Mbunge wa Jimbo la Biharamulo, Eng. Ezra Chiwelesa aliyetaka kujua Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Vituo vya Afya vya Rukaragata, Kalenge na Nyabusozi – Biharamuro 

Dkt. Dugange amesema vituo vya Afya vya Rukaragata, Kalenge na Nyabusozi ni miongoni mwa vituo vya muda mrefu na miundombinu yake inahitaji maboresho kulingana na mahitaji ya sasa

Amesema Halmashauri ya Wilaya ya Biharamuro imetengewa shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa vituo vya afya viwili kati ya vitatu vyenye mahitaji

Aidha, Dkt. Dugange amesema utaratibu wa kutenga bajeti kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa vituo vya afya chakavu ni endelevu