Mtendaji Mkuu Umoja Makampuni ya Bima Tanzania Elia Kajiba
Hayo ameyasema katika mahojiano yake katika kipindi cha Supa Breakfast ambapo amesema kuwa hata katika janga la moto wa Soko la Kariakoo limewaacha na deni la kuwaelimisha umma kuhusiana na bima kwenye biashara zao.
“Tunajaribi kuwasiliana na serikali kama inawezekana sehemu zote za biashara, zenye mikusanyiko mingi kama uwanja wa mpira zote iwe ni lazima kuwekea bima kama ilivyo kwenye magari,” amesema Bw. Elia
Akizungumzia kuhusu kinachokwamisha ukataji wa bima ya biashara amesema; “Kinachotukwamisha ni mtazamo wa wafanyabiashara, inabidi wajue unapokata bima unatakiwa kulipa ada ya bima, lazima tuone tunafanya kitu cha msingi kwa biashara zetu,”amesema Bw. Elia.
Naye Mkurugenzi wa Tafiti na Maendeleo ya Bima, Zakaria Muyengi anesema takwimu zinaonyesha asilimia 36 ya watanzania wanauelewa wa bima huku 15% wanauelewa juu ya matumizi ya bima hivyo kudhihirisha kuwa bado wanakazi ya kufanya.
