Alhamisi , 22nd Mei , 2025

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Haki Afrika Hussein Khalid amesema kuwa Mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi yupo nchini Kenya baada ya kukamatwa Tanzania hivi karibuni

Hussein Khalid alithibitisha kuwa alikuwa pamoja na Mwangi wakiwa njiani kutoka Mombasa na sasa wanaelekea Nairobi.

Waziri Mkuu na Katibu wa Baraza la Mawaziri Musalia Mudavadi, awali alikuwa pia ametangaza kuachiliwa kwa mwanaharakati huyo karibu na eneo la mpaka kati ya Tanzania na Kenya ambaye alikuwa amekamatwa nchini Tanzania kwa siku kadhaa. #EastAfricaTV