
Rais John Pombe Magufuli
Bulaya ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam juu maamuzi yaliyotolewa na Rais Magufuli baada ya kurejesha matumizi ya kanuni za awali za vikokotoo.
"Mnajua kauli ya Rais sio sheria, kwa sababu kulikuwa na sheria ambayo ilipitishwa bungeni na sisi tulipinga, na kile alichokifanya ni huduma ya kwanza tu lakini kinachotakiwa sasa ni kurudisha sheria bungeni ili yatekelezeke" amesema Bulaya.
Ameongeza kwamba "Lisiishie kutoa tamko la Rais, bali aagize yaje yafanyiwe marakebisho bungeni ili jambo liondolewe, na iletwe bungeni kwa hati ya dharura ili isiishie maneno tu kutakuwa na kigugumizi kwenye kulitekeleza,".
Disemba 28, 2018 alipokutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), vyama shiriki, watendaji wakuu wa mifuko ya Hifadhi ya jamii ya PSSSF na NSSF na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) ili kujadili kwa pamoja kuhusiana na mjadala wa kikokotoo kipya cha mafao kwa wastaafu ambapo aliagiza kanuni za awali ziendelee kutumika katika kipindi cha mpito.
"Nimeamua tuwe na kipindi cha mpito, nimeamua kikokotoo kilichokuwa kinatumika kabla ya mifuko kuunganishwa kiendelee katika kipindi cha miaka yote ya mpito. Kipindi cha mpito ni hadi mwaka 2023," alisema Rais Magufuli.