Jumatano , 25th Mar , 2015

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha kwa kauli moja muswada wa sheria ya kudhibiti UKIMWI wa mwaka 2014, ili kuiongezea makali na nguvu sheria iliyoundwa mwaka 2001 ambayo ilipitishwa kama suala la dharura.

Awali akiwasilisha muswada huo bungeni Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mh. Jenista Mhagama, amesema licha ya tume iliyoundwa na kusaidia kupunguza maambuki ya UKIMWI nchini, tume hiyo imekumbwa na changamoto za utekelezaji katika kudhibiti kuenea kwa maambukizi.

Mh. Mhagama amesema pamoja na mafanikio ya sheria hiyo ya mwaka 2001 kupunguza ongezeko la UKIMWI toka asilimia 7 mwaka 2001 hadi kufikia asilimia 5 mwaka 2012 lakini changamoto kubwa iliyopo ni mapungufu ya sheria hiyo katika utekelezaji wa majukumu ya tume iliyoundwa na sheria hiyo.