Jumamosi , 14th Aug , 2021

Ofisi ya Bunge imetoa ufafanuzi juu ya taarifa za upotoshaji zinazosambaa mitandaoni zinazodai wabunge ambao hawatachanja chanjo ya COVID-19,  hawatoingia Bungeni na kusema kwamba upo utaratibu maalum utakaowezesha wabunge wote kuchanja.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taarifa hiyo imetolewa leo Agosti 14, 2021 na kuongeza kuwa kufuataia utaratibu uliowekwa na ofisi hiyo hivyo wabunge wanasisitizwa kutumia hiari kujitokeza kupata chanjo kwa ajili ya kujikinga wao na wale wanaowazunguka.