Jumatatu , 25th Aug , 2025

Operesheni hiyoya Jumamosi Agosti 23, 2025 ilikuwa sehemu ya msako wa kiongozi wa genge anayejulikana kama Babaro, ambaye amehusishwa na shambulio la wiki iliyopita kwenye msikiti mmoja katika mkoa huo.

Maafisa nchini Nigeria wamesema jeshi la anga limeokoa waathiriwa 76 wa utekaji nyara, wakiwemo wanawake na watoto kufuatia  shambulio la anga walilolifanya dhidi ya ngome ya majambazi huko Pauwa Hill kaskazini-magharibi mwa Jimbo la Katsina.

Operesheni hiyoya Jumamosi Agosti 23, 2025 ilikuwa sehemu ya msako wa kiongozi wa genge anayejulikana kama Babaro, ambaye amehusishwa na shambulio la wiki iliyopita kwenye msikiti mmoja katika mkoa huo.

Angalau mtoto mmoja alipoteza maisha wakati wa operesheni ya uokoaji lakini maafisa hawakusema ikiwa kulikuwa na majeruhi wengine kati ya waathiriwa wa utekaji nyara au wanachama wa genge.

Shambulio hilo la anga linaweza kuashiria mafanikio katika juhudi za kusambaratisha mitandao ya wahalifu kaskazini-magharibi mwa Nigeria ambapo magenge yenye silaha yamekuwa yakitesa jamii za vijijini kwa miaka mingi.

Mapema mwezi huu, jeshi la anga lilisema limewaua takriban wapiganaji 35 wa Kiislamu kaskazini-mashariki karibu na Cameroon. Hii ilikuwa ni sehemu ya kampeni iliyoimarishwa ambayo imeshuhudia karibu wanamgambo 600 waliojihami wakiuawa katika kipindi cha miezi 8 iliyopita.