Jumamosi , 4th Mar , 2023

Burundi kupeleka wanajeshi 100 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kama sehemu ya kikosi cha Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC)

Afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Burundi alisema siku ya Ijumaa (Machi 3) kuwa wanajeshi wa nchi hiyo wangelielekea Goma siku ya Jumamosi

Wanajeshi hao wanatazamiwa kupelekwa Kitshanga na Kilorirwe, maeneo yanayodhibitiwa na M23 katika jimbo la Kivu Kaskazini, pamoja na mji wa Sake.Taarifa ya EAC ilithibitisha kupelekwa Kongo wanajeshi wa Burundi.

Kwa mujibu wa ratiba mpya iliyopitishwa na viongozi wa jumuia hiyo, makundi yote yenye silaha, likiwemo la M23, yanapaswa kuondoka ifikapo Machi 30, kufuatia mchakato wa hatua tatu ambao ulipaswa kuanza Februari 28.