Jumapili , 24th Aug , 2025

Céline Ratsiraka aliwahi kuongoza Procoop, mfuko wa uwekezaji chanzo cha ujenzi wa viwanda na miradi ya ushirika ya kilimo nchini Madagascar.

Mke wa rais wa zamani wa Madagascar Didier Ratsiraka, Céline Ratsiraka amefariki siku ya  Ijumaa, Agosti 22, 2025, huko Antananarivo akiwa na umri wa miaka 87.

Celine anakumbukwa na wengi nchini kwake kwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kufanya hali ya talaka kuwa sawa kwa wanawake wa Madagascar kati ya  mwaka 1975 hadi 1993 na tena kuanzia mwaka 1997 hadi 2002 akiwa mke wa rais, kipindi mmewe akiwa madarakani.

Céline Ratsiraka pia alikuwa anaongoza tawi la wanawake la chama cha siasa cha Arema, kilichoanzishwa na Didier Ratsiraka. Wakati wa mapinduzi ya kisoshalisti yaliyotetewa na mumewe mwaka wa 1975, yeye na tawi hili la wanawake walianzisha mtandao wa vituo vya kulelea watoto vya jamii vilivyoitwa Akanin-jaza ili kuwawezesha akina mama kufanya kazi.

Alikuwa pia mhamasishaji wa wanawake kujihusisha na siasa,akiwatia moyo kuwa na mwamko wa kisiasa na kujiunga na mapinduzi ya kijamaa, mapinduzi ambayo yalitetea usawa. Akiwa na dada yake Hortense, waliwakilisha mrengo wa kimaendeleo zaidi wa chama na walisimama dhidi ya wahafidhina wenye msimamo mkali.

Céline Ratsiraka pia aliongoza Procoop, mfuko wa uwekezaji chanzo cha ujenzi wa viwanda na miradi ya ushirika ya kilimo nchini Madagascar.