Ruben Amorim
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imeeleza kuwa, uamuzi huo umefanywa asubuhi ya leo Jumatatu, Januari 5 huku Darren Fletcher akitarajiwa kuiongoza timu kwa muda kama kocha wa mpito.
Katika kipindi chake Old Trafford, Amorim ameiongoza Man United katika mechi 63, akipata ushindi 25, sare 15 na kupoteza mechi 23.
Uongozi wa klabu hiyo ya Old Trafford unaamini mabadiliko hayo ni muhimu na yataleta mabadiliko ya matokeo ya timu.

