Alhamisi , 31st Jul , 2025

Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney amesema Canada inapanga kulitambua taifa la Palestina mwezi Septemba, na kuwa taifa la tatu la G7 kutoa tangazo hilo katika siku za hivi karibuni.

Carney alisema hatua hiyo inategemea mageuzi ya kidemokrasia, ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya Palestina kufanya uchaguzi mwaka ujao bila Hamas.

Matamshi yake yanakuja siku moja baada ya Uingereza kutangaza kulitambua taifa la Palestina mwezi Septemba isipokuwa Israel ikikubali kusitisha mapigano na masharti mengine na hii inakuja wiki moja baada ya Ufaransa kufichua mpango sawa na huo.

Wizara ya mambo ya nje ya Israel ilipinga tangazo la Canada, na kuliita "zawadi kwa Hamas". Nchi nyingi - 147 kati ya nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa - zinalitambua rasmi taifa la Palestina.

Carney alisema Canada italitambua rasmi taifa la Palestina katika Mkutano Mkuu ujao wa Umoja wa Mataifa.
Rais wa Marekani Donald Trump ameonya kuwa uamuzi wa Canada wa kulitambua taifa la Palestina unaweza kufanya mazungumzo ya makubaliano ya kibiashara na Marekani kuwa magumu zaidi.

Israel pia imeikosoa Canada, ikiita hatua hiyo "zawadi" kwa Hamas. 
Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X-Net, Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel ilisema: "Kutambua taifa la aina hiyo kutaathiri juhudi za kufikia usitishaji vita huko Gaza na pia kutazuia mchakato wa kuwaachilia mateka waliosalia.