
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Daud Yasini
Hatua hiyo imekuja kufuatia uamuzi uliofanywa na Rais Samia wa kuruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa
"Chama cha Mapinduzi tunatoa wito kwa vyama vingine vya siasa kuungana na CCM kumpongeza Rais Samia kwa maelekezo aliyoyatoa, lakini pia kuzingatia yale yote Rais aliyoyazungumza, Taifa letu mpaka sasa amani na utulivu vipo vya kutosha, na shughuli za maendeleo zinaendelea," amesema Mwenyekiti huyo.
CCM Iringa imesema kwamba baada ya vyama vya siasa kuruhusiwa kufanya mikutano ya kisiasa hawatarajii kuona uwepo wa vurugu na uvunjifu wa amani Iringa na Tanzania kwa ujumla.