Jumapili , 5th Feb , 2023

Makam wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmshauri kuu ya CCM Taifa Dkt. Philip Isdor Mpango amesema CCM ni chama cha wanyonge na kuwataka viongozi wa chama hicho kuwatetea wananchi, kusikiliza changamoto  na kuzipatia ufumbuzi.

Mpango amesema hayo mkoani Pwani wakati akizungumza na viongozi wa chama hicho  katika Ukumbi wa Shule ya Uongozi wa Mwalimu Nyerere iliopo Kibaha na kusema kuwa dhumuni la kuanzishwa kwa chama hicho ni ni kutetea na kuwasemea wanyonge hivyo kinapaswa kukemea maovu na uonevu, kuwasemea wananchi na kubeba ajenda za wananchi kuanzia ngazi ya Shina hadi Taifa

.
“Chama chetu kilianzishwa kwa ajili ya kutetea na kuwasemea wanyonhe CCM ni chama cha ukombozi,chama cha wafanyakazi na wakulima ni chama cha watu kisikae kimya katika kukemea maovu”
Dkt. Mpango pia  ameiagiza Wizara ya Nishati kupitia shirika la umeme TANESCO kuhakikisha wanashirikiana na wananchi kutatua kero zote zitokanazo na ujenzi wa miradi ya Nishati mkoani Pwani