
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka
Kauli hiyo imetolewa hii leo Septemba 8, 2022, na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka, jijini Dar es Salaam, wakati akitoa taarifa ya maazimio ya kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM iliyoketi hapo jana kufuatia uwepo wa malalamiko ya wananchi kuhusu tozo za miamala ya simu na kibenki.
"Niwaombe Watanzania wawe watulivu, chama chao ambacho kimekuwa kikisimama nao katika nyakati zote kiko makini na kimeendeleo kufuatilia kwa ukaribu sana vikwazo hivi, misingi ya chama chetu haiamua jambo barabarani, linapotokea jambo tunakutana, linajadiliwa kwa kina na kwa utaratibu ni wakati muafaka kwa CCM kukutana nakutoa kauli hii kwa Watanzania" amesema Shaka.
Aidha CCM imetoa maelekezo kwa serikali, "Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa, imeielekeza serikali kutazama hali halisi na kuchukua hatua stahiki kuhusu maoni na ushauri wa wananchi kuhusu tozo, ".