CHADEMA yasusia uchaguzi

Alhamisi , 7th Nov , 2019

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza kutoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa huku wagombea wake wagombea wake kutokata rufaa.

Freeman Mbowe ametangaza uamuzi huo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, baada ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika leo, ambapo amedai hawakubaliani na sababu za wagombea wa chama hicho kukatwa.

Sisi kama chama tumeamua hatutashiriki zoezi hili na ninatoa amri kama Mwenyekiti wa viongozi na wagombea nchi nzima wasitishe kugombea na wasitishe kukata rufaa." amesema Mwenyekiti Mbowe

Mbowe ameongeza kuwa “waachane na kuweka mapingamizi hatupo tayari kubariki ubatili, huu ni uhuni, wananchi wana hasira na wana haki ya kuwa na hasira na waendelee kuwa na hasira,” 

Novemba 24, 2019 watanzania watashiriki zoezi la kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa.