Jumatano , 8th Mar , 2023

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa maridhiano ya kuboresha na kuimarisha demokrasia nchini yenye amani, upendo na mshikamano.

Rais Samia akipokea tuzo ya maridhiano kutoka kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe

Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa BAWACHA Catherine Ruge, wakati Rais Samia akikabidhiwa tuzo ya maridhiano na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe aliyeikabidhi kwa niaba ya Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) mara baada ya kuwahutubia kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Moshi mkoani Kilimanjaro leo Machi 8, 2023.

Tazama video hapa