Jumatano , 1st Mar , 2023

Mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila, amemtaka mkuu wa idara ya mipango miji, Manispaa ya Bukoba na Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoani humo, kuainisha viwanja ambavyo watu walipewa tangu miaka ya 90 na havijaendelezwa, vipelekwe kwenye mamlaka ya Rais kuvifuta.

Mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila,

RC Chalamila amesema kuwa viwanja hivyo vinapaswa kufutwa ili waweze kumilikishwa watu wengine kwa masharti ya kuviendeleza na kubadilisha mji.

Akizungumza katika kikao cha kujadili maendeleo ya mkoa Chalamila amesema kuwa uwepo wa viwanja hivyo visivyoendelezwa, mbali na kukwamisha maendeleo ya kiuchumi pia vinaufanya mji kuonekana ni magofu na usioendelea.

"Kiwanja kimechukuliwa miaka yote hiyo, hakiuzwi na wala hakiendelezwi, kwahiyo Kamishna wa Ardhi Msaidizi na watu wa ardhi wa Bukoba, wafanyie kazi haya ili tuweze kwenda nayo kwa haraka, kwa mfano viwanja vingine vipo hapa Kashura vinautazama mji, ni kuvifuta na vikishafutwa wamilikishwe watu wengine kwa masharti ili mji wetu uweze kukimbia kwa haraka kimaendeleo" amesema Chalamila.