CHAWATA wamlilia Mkapa

Jumatatu , 27th Jul , 2020

Chama cha Walemavu Tanzania (CHAWATA) kimeelezea namna rais wa serikali ya awamu ya tatu hayati Benjamin William Mkapa aliivyokuwa mstari wa mbele katika kujali maslahi ya kundi hilo kwa kusaini mkataba ambao ulikuwa na tija kwa jamii ya walemavu.

Hamad Abdallah Komboza Mwenyekiti CHAWATA

Chama cha Walemavu Tanzania (CHAWATA) kimeelezea namna rais wa serikali ya awamu ya tatu hayati Benjamin William Mkapa aliivyokuwa mstari wa mbele katika kujali maslahi ya kundi hilo kwa kusaini mkataba ambao ulikuwa na tija kwa jamii ya walemavu.

Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho Hamad Abdallah Komboza amesema hayati Benjamin William Mkapa alifanikiwa katika kuhakikisha watu wenye ulemavu wanakuwa na miundo mbinu rafiki ya kuwawezesha kupata elimu sawa na jamii nyingine..

Amesema hayati Benjamin William Mkapa pia aliwawezesha watu wenye ulemavu kwa kuwashirikisha kwenye uundwaji wa sera mbalimbali za maendeleo ya nchi.."Hatuwezi kumsahau marehemu Mkapa uongozi wake umekuwa thabiti katika kipindi chote hakika tutamkumbuka sana"