Jumatatu , 12th Oct , 2015

Mgombea urais wa Zanzibar kwa chama cha wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amewahakikishia wakulima serikali yake ikipata nafasi ya kuongoza itaweka mazingira mazuri wakulima na wajasiriamali kujiendeleza na kufaidika kimaslahi.

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa chama cha wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad

Mgombea huyo wa urais ametoa ahadi hiyo huko Kiembeni Dunga mkoa wa Kusini Unguja katika mkutano wa kampeni za urais wakati akiwahutubia wakazi wa majimbo ya uzini na Tunguu.

Maalim Seif ameongeza kuwa sekta hiyo ya wakulima na wajasiriamali imeachwa ikizorota na serikali imekuwa haiwapi msukumo unaohitajika hivyo serikali yake itaiboresha sekta hiyo ikiwemo kujenga benki kwa ajili ya wakulima na wajasiriamali.

Mgombea huyo wa urais ambaye pia ni makamu wa kwanza wa rais na katibu mkuu wa cuf taifa alizugumzia hali ya elimu kwa vijana wa zanzibar ambapo amemsmea akiwa rais seriklai yake itaweka mfumo mzuri wa elimu ambao utawapunguzia mzigo wazazi na vijana wengi kuendelea.