Ijumaa , 16th Nov , 2018

Chama Cha Wananchi wa CUF upande wa Profesa Lipumba umefunguka kuwa waliokuwa wabunge wake na baadaye kuhamia Chama Cha Mapinduzi kwa kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kuwa ifikapo 2020 wabunge hao wataondolewa kwenye kura za maoni.

Mbunge aliyejiuzulu Abdallah Mtolea na Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama Ibrahim Lipumba.

Kauli hiyo ya CUF imetolewa na Mkurugenzi wa Habari Abdul Kambaya ikiwa ni siku moja tangu Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdallah Mtolea atangaze kujiuzulu nafasi yake ubunge na baadaye kutangaza kuingia Chama Cha Mapinduzi.

Hawa wakina Polepole, wanasema wazi kwamba hii ofa ya dirisha dogo itaishia 2020 baada ya hapo utaratibu wa CCM utafuatwa, sidhani kama wataweza mikiki kwa sababu wagombea Urais wanapanga safu zao, niwaombe wanachama wetu wawe watulivu kwani CUF yetu sio mtu bali ni sera na misingi.”

Tatizo kubwa wanaohama sasa wanadhani kuwa wanaweza kuwa Waitara, (Uwaziri) washatoka kwenye fikra za kutaka kuwa wabunge tena ila wanachowaza ni kuwa Mawaziri, na ndiyo maana unaona kuna ongezeko kubwa la watu kuhama.”

Jana wakati wa muendelezo wa vikao vya Bunge Jijini Dodoma Abdallah Mtolea alitangaza kujiuzulu kwa nafasi yake ya ubunge kwa kile alichokidai kuwa kukwepa migogoro ya kiuongozi baina ya upande wa Mwenyekiti wa anayetambuliwa na Msajili wa Vyama nchini Profesa Lipumba na Katibu Mkuu wake Maalim Seif Sharif Hamad.