
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba
Prof. Lipumba amesema hayo leo, wakati akizungumza na vyombo vya habari Jiji Dar es Salaam, ambapo baraza la chama hilo limemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu kujiwekea lengo la kushinda tuzo ya Mo Ibrahim kwa kujenga Demokrasia, kuongoza serikali yenye utawala bora, kuheshimu haki za binadamu na kukuza uchumi shirikishi.
"Baraza Kuu la CUF limehuzunishwa na ukosefu wa furaha kwa Watanzania, umasikini na uvuinjifu wa haki za binadamu umewafanya Watanzania wasiwe na furaha katika maisha yao, taarifa ya furaha dunia 2021 inaonyesha Tanzania ni ya 94 kati ya nchi 95, bakora za CCM zimetufanya tuwe taifa la watu walionuna hata ukimtekenya mtu kucheka ni shughuli kubwa," amesema Prof. Lipumba.
Awali akaizungumza kuhusiana na masuala ya uchumi Prof. Lipumba ameeleza kuwa Baraza Kuu la CUF limebaini kupungua kwa ukuaji wa pato la viwanda kutoka asilimia 10.8, mwaka 2016 hadi kufikia asilimia 5.8 kwa mwaka 2019.
"Baraza Kuu limebaini Tanzania ya viwanda bado ni ndogo, ajira katika viwanda vyote ni chini ya watu 340,000 kwenye nchi ambayo ina nguvu kazi zaidi ya watu milioni 27, ukuaji wa pato la viwanda umepungua kutoka 10.8% mwaka 2016 kufikia 5.8% 2019," amesema Prof. Lipumba.