Jumanne , 25th Aug , 2020

Jiji la Dar es salaam limetajwa kuzalisha taka zaidi ya tani 5300 ambazo zinazokusanywa ni takribani asilimia 40 hadi 50 hivyo wadau, mbalimbali vijana wamehimizwa kulitazama suala hilo Kama fursa inayoweza kuwaongezea kipato.

Sehemu ya takataka zinazozalishwa ndani ya jiji la Dar es Salaam

Rai hiyo imetolewa na afisa mazingira kutoka ofisi ya Makamu wa Rais mazingira DK Hussein Omary katika kikao Cha wadau wa Mazingira kilichopewa jina la Taka ni Ajira ambaye amesisitiza kuwa kwenye eneo Hilo kwa jiji la Dar es Salaam pekee Takataka za Plastic ambazo hazijalejelezwa zinakaribia zaidi ya dola za Marekani milioni 20.

Bado kuna fursa kubwa  katika masuala ya takataka sheria zipo kanuni ziko wazi kuliko kuwazuia vijana kukusanya taka ni bora kujengea Mfumo ili watambulike na waweze kujipatia kipato" alisema DK Hussein Omary Afisa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais.

Aidha kongamano hilo limelenga kueleza jinsi kijana anavyoweza kujiajili katika sekta ya mazingira kwa kuchagua kukusanya taka ngumu au za plastiki ambazo anaweza kuuza na kujiongezea kipato.

Licha ya serikali kuweka mikakati ya kutokomeza takataka imeombwa pia kurekebisha baadhi ya sera kanuni ili vijana wanazoweza kujiunga kukusanya taka mitaani watengewe eneo maalum la kuzikusanya wakitambuliwa na mifumo Rasmi katika Halimashauri mbalimbali Nchini.