Jumamosi , 18th Apr , 2020

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo kupitia kipindi cha SupaBreakfast amesema hajazuia wamiliki kufungua Baa zao, bali alichozuia ni watu kujaa kwenye baa.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo.

Akizungumza kwenye kipindi hicho, Daniel Chongolo amesema si kweli amepiga marufuku kufungua baa, na wala hakuagiza wanancchi kuchapwa bakora na Polisi, bali wanachofanya kuepusha misongamano.

'Hakuna aliyezuiliwa kufungua bar kilichozuiwa ni watu kujaa kwenye Baa sasa kama hawawezi kufanya kazi bila watu kukusanyika hilo ni jambo jingine' amesema Chongolo

Kuhusiana na na polisi kuwapiga bakora, Chongolo amesema kuwa "wanaendaje kupiga watu wanaowakuta baa, mikusanyiko isiyo ya lazima ndiyo iliyozuiwa tunapokuta watu wamekusanyika bila kuwa na sababu za msingi tutawatawanyisha"