Alhamisi , 7th Jul , 2022

Mkuu wa wilaya ya Kigoma Ester Mahawe ameagiza mamlaka ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Kigoma, kufanya uchunguzi katika mradi wa Zahanati ya kijiji cha Samwa kata ya Kidakhwe wilayani Kigoma kufuatia mradi huo kutumia gharama kubwa na kupitiliza muda wa utekelezaji 

Agizo hilo amelitoa baada ya kamati ya siasa chama cha mapinduzi wilaya ya kigoma kufanya ziara kijijini hapo, ambapo wananchi wamelalamika mradi huo kushidwa kukamilika kwa wakati licha ya kuendelea kukosa huduma za matibabu karibu.

Awali kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Kigoma Erasto Kitabi alieleza mradi huo kusuasua kutokana na mkandarasi anayesimamia kutokuwa na uhusiano mzuri na kamati ya ujenzi licha ya kupewa fedha zote za mradi kiasi cha shilingi milioni 70