
Msanjila ambaye pia alikuwa ni dereva wa bodaboda alikutwa na mauaji hayo Februari 19 mwaka huu ambapo alitoka kwenda kwenye kazi zake lakini hakurudi mpaka alipookotwa Februari 21 mwaka huu akiwa ameuawa.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, David Misime Mwili wa Msanjila uliokotwa kwenye mlima wa Isanga maeneo ya magereza katika Manispaa ya Dodoma majira ya saa 12:30 jioni.
Kamanda Misime amesema kuwa awali kabla ya kifo chake Alfred Msanjila alikwenda eneo lake la kazi kituo cha Bodaboda mtaa wa Uzunguni Club lililoko Kata ya kizota na hakuweza kurejea nyumbani wala haikujulikana alipo.
Misime ametoa wito kwa wananchi wasikubali kununua au kupewa pikipiki ambayo hawajahakiki uhalali wake TRA, Polisi na Mamlaka zingine, pia amewataka viongozi wa Serikali za mitaa nao wawe makini katika kusimamia mauziano ya aina yoyote ile kwani inaweza kupelekea kuhusishwa na tukio hili.