Dk. Shein atunuku nishani zilizotukuka 43 

Ijumaa , 12th Jan , 2018

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein ametunuku nishani zilizotukuka 43 kwa viongozi na watumishi wa umma ikiwa ni maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

Dkt. Shein ametoa nishani hizo kwa mutu ambae aliasisi,alishiriki na kutukuza pamoja na kuyaenzi Mapinduzi ya Zanzibar yaliyotokea mwaka 1964.

Pamoja na hayo Dk. Shein amewataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo ili kuwa chachu ya kuendelea kuwa kivutio kikubwa kwa uwekezaji miradi mikubwa ya maendeleo visiwani .

Katika maadhimisho hayo mbali ya nishani hizo serikali ya Zanzibar huzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni ishara ya ukombozi wa fikra na maendeleo ya kiuchumi ya taifa hilo.