Ijumaa , 29th Apr , 2022

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, amehudhuria ibada ya kitaifa ya kuagwa kwa mwili wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu wa nchi ya Kenya Hayati Mwai Kibaki.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.

Ibada hiyo ya kuagwa kitaifa, imeongozwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, na kuhudhuriwa na Wakenya, viongozi  wa nchi hiyo pamoja na viongozi wa nchi kutoka mataifa mbalimbali akiwemo Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na Rais wa Ethiopia Sahle-Work Zewde.

Mwai Kibaki, alifariki dunia Aprili 22, 2022 akiwa na umri wa miaka 90.