Jumatano , 28th Oct , 2020

Rais wa Zanzibar, anayemaliza muda wake Dkt.Ali Mohammed Shein amewaomba wananchi ambao bado hawajapiga kura wajitahidi kuwahi ili wapate nafasi ya kuwachagua viongozi wanaowataka

Rais wa Zanzibar, anayemaliza muda wake Dkt.Ali Mohammed Shein akiwa anapiga kura leo visiwani Zanzibar.

Dkt.Shein, amesema hayo leo visiwani Zanzibar, baada ya kumaliza kupiga kura huku akisema  kuwa baada ya kusikiliza kampeni za siasa tayari muda umefika wa wananchi kukamilisha maamuzi yao.

“Nataka niwahakikishie wananchi kwamba wao wote ambao hawajaja kwenye vituo vya kupiga kura wajitahidi waje mapema sana ili wapate nafasi ya kuwachagua viongozi ambao wanawataka wao wenyewe” amesema Dr.shein

Aidha Dkt.Shein amewatoa hofu kwa kuwahakikishia kuwa hali ya vituo vya kupigia kura ni salama na kuna ulinzi wakutosha kwa ajili ya usalama.

“Hawatakiwi wawe na hofu wapo nchini kwao, wako huru,hii ni serikali yao, wanachagua viongozi wengine wa serikali wapya badala ya sisi tunaomaliza muda wetu” amesema Dkt.shein