Dodoma watekeleza agizo la Magufuli kwa haraka

Jumamosi , 30th Nov , 2019

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, amesema utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ulipaji wa fidia wa eneo la Kikombo lililochukuliwa na Jeshi, kwa ajili ya kujenga Makao Makuu ya Ulinzi yanaanza wiki ijayo.

Rais Magufuli

Mkurugenzi huyo amesema kama maelekezo yalivyotolewa tayari taratibu zote zimeshakamilika ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa fedha na kinachofanyika kwa sasa ni uhakiki wa wananchi wanaopaswa kilipwa.

Amesema kuwa zoezi ambalo linaratibiwa na Wizara ya Fedha linaenda sambamba na ufunguaji wa akaunti za malipo kwakuwa watatumia mfumo wa Serikali wa Kibenki katika kufanya malipo hayo ya fidia ili fedha hizo ziwe salama.

Eneo lote linaukubwa wa hekari 5000, eneo linalokusudiwa kwaajili ya kulipwa fidia ni hekari 3431 na wanufaika wa fidia hiyo ni wananchi 1526, ambao wanapaswa kulipwa fidia Bilioni 3, kuhusu ujenzi wa barabara wa Kilomita 18 kuelekea Makao Makuu hayo nalo zoezi linaendelea kwa kasi.