Jumatatu , 1st Jun , 2015

Viongozi wa nchi za Afrika Mashariki wamemtaka Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza kuahirisha uchaguzi uliopangwa ifanyika nchini humo mwezi Juni na kutaka kusitishwa kwa vurugu zilizoibuka baada ya kiongozi huyo kuamua kuwania muhula wa tatu

Viongozi wa nchi za Afrika Mashariki wamemtaka Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza kuahirisha uchaguzi uliopangwa ifanyika nchini humo mwezi Juni na kutaka kusitishwa kwa vurugu zilizoibuka baada ya kiongozi huyo kuamua kuwania muhula wa tatu wa kuliongoza taifa hilo.

Taarifa iliyotolewa jana mara baada ya kikao cha viongozi hao kilichofanyika jijini Dar es salaam pia viongozi hao wametaka kuvuliwa kwa silaha kwa makundi ya vijana na sharti la kurejea kwa wakimbizi nchini humo.

Takribani watu 90 raia wa Burundi wamekimbia nchi hiyo kufuatia vurugu hizo na msemaji wa serikali ya Burundi Philippe Nzobonariba ameliambia shirika la utangazajI la AFP kuwa serikali huyo imeipokea taarifa ya viongozi hao ya kutaka kuahirishwa kwa uchaguzi nchini humo.

Hata hivyo suala la Rais Nkurunziza atawamia muhula wa tatu halikujadiliwa katika mkutano huo na hivyo serikali ya Burundi inachukulia suala hilo kuwa mjadala wake umefungwa.

Tags: