
Warren Bright, Mkuu wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani kwa upande wa Tanzania (UNFPA)
Kauli hiyo ameitoa hii leo Machi 13, 2021, wakati akizungumza kwenye kipindi cha MadiniDotCom kupitia East Africa Radio kinachoruka kila siku ya Jumamosi saa 9:00 Alasiri hadi saa 10:00 jioni, na kusema kuwa shirika hilo linapinga masuala ya ukatili na unyanyasaji hivyo hawawezi kutoa nafasi kwa mtu ambaye anafanya hayo.
"Kuna wasanii wanaamini katika kiki mimi katika uongozi wangu siwezi kuamini katika kiki, kama ninavyosema 'portfolio' yangu ni kubwa katika shirika ninalofanyia kazi tukiingiza kiki siku zote inaingia kwenye mambo ya unyanyasaji wa kijinsia kwa upande wa watoto wa kike, kwahiyo msanii anapoona kwamba kumtumia msichana au mwanamke kwake yeye ni kitu ambacho kina-trend kumbuka mimi napinga hilo,"amesema Warren
Aidha Warren ameongeza kuwa, "Msanii hatuwezi tukakutumia wewe kuwa kama balozi au champion wetu lakini nyuma ya pazia ukitoka unaanza kutukana na kuwanyanyasa wanawake, wasanii wahakikishe wanajiepusha na vitendo vya kiki na vile vitaweza kumuingiza kwenye matatizo ya ukatili wa kijinsia"