
Pichani Ibraah na Diamond
"Kama kuna chochote kinaendelea basi mtakiona kwasababu hakuna kitakachojificha kwasababu ni kazi na tunapofanya kazi siku zote tunahitaji umoja kwahiyo kama itatokea mtaona hatutoficha chochote'' Amesema Ibraah
"Siwezi kuficha chochote kama Wcb Wasafi ndio sehemu nitakayoenda mtaona kwasababu ndio nitakuwa nafanya nao kazi lakini kwasasa tupo Oya Gang" Amesema Ibraah
Ikumbukwe kuwa Msanii Ibraah ameachana na label yake ya zamani Konde Gang siku za hivi karibuni na kutambulisha uongozi wake mpya ambao unaitwa Oya Gang